Mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide atawasili nchini leo Jumamosi kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi, Jumapili pale uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Kama hujakata tiketi wakati ni huu, kwani tiketi zinauzwa kwa kasi ya 'kimbunga'
Tiketi za Royal zimemalizika ambapo mpaka kufikia mchana wa leo Ijumaa, jumla ya tiketi 47, 863 zimeshauzwa
Uwanja wa Benjamin Mkapa unachukua takribani mashabiki 60,000 hivyo kuna takribani tiketi 13,000 zilizosalia
Kwa hakika Benjamin Mkapa hapatatosha siku ya Jumapili...!

ADVERTISE HERE