Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi, amejiunga na klabu ya Geita Gold iliyopanda ligi kuu msimu uliopita
Mahadhi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Geita Gold
Tangu apone majeraha yaliyomuweka nje msimu mzima, Mahadhi ameshindwa kurejea katika kiwango chake kilichompa sifa alipojiunga na Yanga msimu wa 2016/17
Hii ni nafasi kwake kujiimarisha, amehitaji timu itakayomuhakikishia nafasi ya kucheza mara kwa mara
Aidha, wakati Mahadhi akitua Geita Gold, kiungo kutoka Zanzibar Abdulaziz Makame 'Bui' yeye amesajiliwa na Namungo Fc
Mkataba wa Makame na Yanga ulimalizika mwishoni mwa msimu huu, miezi sita ya mwisho akitumika kwa mkopo kunako klabu ya Polisi Tanzania
ADVERTISE HERE