Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema wanasubiri hukumu ya shauri la mchezaji Bernard Morrison raia wa Ghana akiamini hukumu hiyo itatolewa wakati wowote
Mfikirwa amesema baada ya shauri hilo kusikilizwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), walitaarifiwa kuwa hukumu hiyo ingetoka hadi kufikia August 24
"Kesi hii imechukua muda mrefu, sisi viongozi tumekuwa tukiwasiliana na CAS kupitia email. Kila mmoja ana shauku ya kufahamu maamuzi ya kesi, ni hivyo hata kwa sisi viongozi"
"Siku ya jana (juzi) mimi sikulala, kila wakati nilikuwa nikifungua Email ya klabu kuona kama kuna taarifa kutoka CAS. Kwa sasa kesi hiyo imemalizika, sisi viongozi hatuna la kufanya zaidi ya kusubiri hukumu"
"Hii ni Mahakama inafanya kazi kwa utaratibu wake, hata kama walituahidi kuwa wangetoa hukumu August 24, sisi viongozi hatuwezi kuanza kuwauliza kwa nini hawajatoa hukumu hiyo mpaka sasa. Ninachoamini hukumu itatoka siku yoyote tunapaswa kusubiri," alisema Mfikirwa
Kesi ya mgogoro wa Mkataba kati ya Yanga dhidi ya Morrison ilisikilizwa Julai 29 kwa njia ya mtandao ambapo CAS wakaahidi kuwa wangetoa hukumu hadi kufikia August 24