Manara ataongeza nguvu kitengo cha Uhamasishaji - Mfikirwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2021
Manara ataongeza nguvu kitengo cha Uhamasishaji - Mfikirwa

Uongozi wa Yanga umeweka bayana majukumu ya Haji Manara aliyetambulishwa juzi akitokea klabu ya Simba

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu nafasi ya 'Bugatti' hasa ikizingatiwa Yanga inae Afisa wa Habari, Hassan Bumbuli na Afsa wa Uhamasishaji Antonio Nugaz

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema Manara ataingia kwenye Kitengo cha Uhamasishaji wakiamini atasaidia kuimarisha kitengo hicho kuelekea Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji

"Wakati tunamtangaza Manara pale Serena Hotel hatukusema anakuja kufanya kazi gani hasa, lakini niseme uongozi upo makini na haujakurupuka kumchukua Haji, kuna majukumu yapo na ataenda kuyafanyia kazi hasa kutokana na mabadiliko ya klabu yanayofanywa sasa, kutoka katika mfumo wa sasa na kwenda mfumo mpya na wa kisasa zaidi, hatoingiliana na Nugaz na Bumbuli" alisema Mfikirwa

"Katika mabadiliko ambayo tunayafanya kwa sasa kuna suala la ‘fan base', hapa tunahitaji mtu wa kushawishi mashabiki waingie kwenye mfumo rasmi wa klabu baada ya kukamilika taratibu zote, kuna mashabiki mikoa mbalimbali ambao klabu inawahitaji, lakini lazima washawishike, hapa ndipo panapohitajika watu au mtu mwenye kujua kushawishi, kuna nani zaidi ya Manara?, ili ni eneo ambalo tunaamini atafanya kazi kubwa sana kwa manufaa ya klabu"

Mfikirwa alisisitiza kuwa kila mmoja (Nugaz, Bumbuli na Manara), atafanya kazi yake kwa maendeleo ya klabu na hakutakuwa na mwingiliano.

"Mashabiki wauamini uongozi wao, sisi tupo pale (madarakani) kwa niaba yao, hivyo chochote tutakachokifanya ni kwa faida ya timu hivyo hakuna haja ya kuwa na shaka na ujio wa Manara ndani ya Yanga"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’