Singida United imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuilaza Mlandege mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Ijumaa mchana.
Mabao ya Danny Usengimana, Kenny Ali na Lubinda Mundia yameihakikishia Singida United nafasi ya nusu fainali licha ya kuwa na michezo miwili mkononi.
Singida United imeshinda michezo yake yote mitatu na kufikisha alama tisa, ikiwa kileleni kundi B.
Baadae Azam FC inayoongoza kundi A itaivaa URA huku mchezo wa mwisho kwa siku ya leo ukiwa wa kundi B ukipigwa saa mbili na nusu usiku kati ya Yanga dhidi ya Taifa ya Jan'gombe.
Simba itashuka dimbani kesho Jumamosi saa mbili na nusu usiku kuikabili Azam FC.

ADVERTISE HERE