Leo Yanga itafanya tukio jingine kubwa pale Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2021/22 zitazinduliwa
Kwa mara ya kwanza, Shoo hiyo ya kibabe itasimamiwa na Bugatti mwenyewe, msemaji mpya wa Yanga Haji Manara
Manara ametamba kuwa Yanga inakwenda kuzindua jezi ya mpira ambayo haina 'makorokoro'
Jezi tatu zitazinduliwa; jezi ya nyumbani, ugenini na jezi ya dharura (third kit)
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema ni utamaduni kwa Yanga kila msimu kutoa jezi bora hapa Tanzania
Jezi inayokwenda kutambulishwa leo, itavunja rekodi kwani ni bora zaidi ya matoleo yaliyopita
Hafla ya uzinduzi itafanyika kuanzia saa tano asubuhi na itakuwa mbashara kupitia Azam Sport 1 HD
ADVERTISE HERE