Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina anatarajiwa kuwasili wikiendi hii akitokea kwao nchini Zambia.
Lwandamina alipata msiba wa kufiwa na mwanawe Mofya Lwandamina mwishoni mwa mwaka jana.
Msiba huo ukimkuta nchini Zambia alikokwenda kwa ajili ya mapumziko wakati ligi kuu ya Vodacom iliposimama kupisha michuano ya kombe la Chalenji.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinabainisha kuwa kocha huyo asiye na maneno mengi anatarajiwa kuungana na kikosi cha Yanga visiwani Zanzibar muda mfupi baada ya kurejea.
Kwa sasa Yanga inayoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi iko chini ya makocha wasaidizi Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa.
Wawili hao wameiongoza Yanga kushinda michezo yote miwili ya kombe la Mapinduzi, mchezo wa kombe la FA dhidi ya Reha FC na kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC.

ADVERTISE HERE