Mwamba ameanza kazi na Wananchi! Baada ya kutambulishwa rasmi kujiunga na Yanga, Haji Manara amesema kazi ya kwanza msimu ujao ni kuhakikisha wanashinda makombe yote ya ndani pasipo kuilalamikia TFF wala Bodi ya Ligi
Akitoa salamu zake za shukrani baada ya kujiunga na Yanga, Manara alikiri kuwa Yanga ndio klabu kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
Aidha Manara amesema usajili uliofanywa na Yanga msimu huu, unampa kila sababu ya kuamini Yanga inakwenda kushinda makombe yote ya ndani
"Nashukuru kujiunga na Yanga mabingwa mara 27 Tanzania, klabu kubwa kuliko zote katika ukanda wa Afrika Mashariki"
"Niwaahidi viongozi, Kamati ya Utendaji na Mashabiki, kuwa msimu ujao tunakwenda kuchukua kombe letu bila kulalamikia Bodi ya Ligi wala TFF"
"Nimeona usajili uliofanyika nawahakikishia tuna timu inayoweza kushinda mataji yote," alitamba Manara
Aidha Haji ambaye Baba yake Mzazi ni Mzee Sunday Manara, mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye sasa ni Mjumbe wa Kamati ya ufundi, amesema atafanya kazi mara 10 zaidi ya vile alivyofanya akiwa na Simba