Timu zilizotoa wachezaji wengi katika timu za Taifa zinakabiliwa na changamoto katika maandalizi yao kuelekea mechi za awali michuano ya ligi ya mabingwa kwa zile timu zinazoanzia hatua ya awali
Yanga imetoa wachezaji nane katika timu za Taifa, wachezaji hao watakosekana kikosini kwa takribani wiki mbili
Ramadhani Kabwili, Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Feisal Salum, Djigui Diarra, Khalid Aucho na Mukoko Tonombe ndio wachezaji waliojiunga na timu za Taifa
Tanzania inaanza kambi ya maandalizi leo kwa ajili ya mechi dhidi ya Madagascar na DR Congo
Mechi za kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia zitapigwa kati ya Septemba 02 na Septemba 09
Septemba 12 mechi za hatua ya awali ligi ya mabingwa zinaanza, kwa maana kuwa hakutakuwa na muda zaidi wa kufanya mazoezi ya pamoja kuelekea mechi za ligi ya mabingwa