Kiungo mpya wa Yanga Khalid Aucho yuko ndani ya mji wa Marrakech nchini Morocco kuungana na wenzake wanaoendelea na kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa michuano ya ndani ya ligi ya mabingwa
Aucho alipewa ruhusu ya kurejea kwao Uganda kukamilisha masuala binafsi baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga
Aidha uongozi wa Yanga pia ulikuwa ukifuatilia ITC yake baada ya klabu ya Al Makassa ya Misri aliyokuwa akiitumikia awali kuchelewa kuitoa
Ndiye mchezaji pakee ambaye alikuwa amebakia kuungana na wenzake Morocco
Mwamba huyu sasa ametua kukamilisha maandalizi kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi August 29 uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE