Kikosi cha Yanga kimewasili mapema leo nchini Morocco tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi na michuano ya Kimataifa
Yanga wameweka kambi katika Kituo cha Soka cha Mohammed VI, kilichopo ndani ya Mji wa Sale
Kituo hicho cha kisasa zaidi nchini Morocco kinamilikiwa na Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF). Kilijengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco, Mohammed VI kwa lengo la kuibua vipaji na kuendeleza michezo
Ndani ya kituo hicho mahitaji yote ya timu yanapatikana. Kina viwanja vinane vya mpira wa miguu. Viwanja hivyo vina urefu zaidi ya mita 120 na vinapunguzwa kutokana na mahitaji ya timu.
Kuna uwanja wa ndani ambao umejengwa kwa ajili ya timu kufanya mazoezi pamoja na hali ya hewa kubadilika.
Kwa hali ya hewa ya Morocco, sio mvua tu inasababisha mazoezi kutoendelea, bali hata jua nalo linasababisha. Hivyo hali hiyo ikitokea timu itafanyia mazoezi kwenye uwanja wa ndani. Uwanja huo pia unatumika kwa ajili ya kozi za makocha, waamuzi na wengineo. Unaingiza zaidi ya watu 1,000
Ni kambi ya kisasa sana kwa Yanga ambayo inagharamiwa na klabu ya RS Berkane ikiwa ni sehemu ya makubaliano katika mauzo ya winga Tuisila Kisinda
Wananchi wataanza kutamba katika maeneo haya kuanzia kesho Jumanne..




