Mwishoni mwa wiki kulikuwa na mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutangaza kuongeza idadi ya nyota wa kigeni kutoka 10 na kuwa 12 huku wakiruhusu wachezaji 8 kutumika kwenye mchezo mmoja katika mashindano ya ndani
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said amesema pamoja na mabadiliko hayo, wao wameridhika na usajili walioukamilisha
Hata hivyo Hersi amesema kama kutakuwa na umuhimu baadae wanaweza kujaza nafasi hizo katika usajili wa dirisha dogo
Ongezeko la nyota wa kigeni lilitangazwa na TFF siku moja kabla ya dirisha la usajili kwa ajili ya michuano ya CAF kufungwa juzi
Wachezaji 10 wa kigeni waliosajiliwa na Yanga ni Djigui Diarra, Shabani Djuma, Yannick Bangala, Mukoko Tonombe na Khalid Aucho
Wengine ni Jesus Moloko, Fiston Mayele, Yacouba Songne, Saido Ntibazonkiza na Heritier Makambo