Yanga imemtambulisha rasmi winga Jesus Ducapel Moloko liyesajiliwa kutoka klabu ya AS Vita kwa mkataba wa miaka miwili
Utambulisho wa mchezaji huyo umerushwa mbashara na Azam Tv ambapo winga huyo amesema amekuja nchini kwa ajili ya jukumu moja tu, kuwapa furaha mashabiki wa Yanga
Aidha Moloko amesema hajawahi kushindwa katika timu zote alizopita akiwahakikishia mashabiki kuwa msimu huu wataweza kutimiza malengo yaliyowekwa
"Nafurahi kujiunga na Yanga, ni timu kubwa Afrika. Nimekuja kuisaidia Yanga kufanya vizuri katika mashindano yote ikiwa ni pamoja na kuingia hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika"
"Nawaambia mashabiki watarajie mambo mazuri kutoka kwangu kwani sijawahi kufeli," alisema Moloko
Moloko ametambulishwa sambamba na mlinzi wa kulia Shabani Djuma