Chirwa aitwa arejee kazini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2018
Chirwa aitwa arejee kazini
Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa bado ameweka ngumu kurejea kuitumikia Yanga licha ya makubaliano ya awali waliyofikia na uongozi wa Yanga.

Chirwa aliahidiwa kulipwa fedha zake za usajili kwa awamu lakini muhimu alitakiwa kurejea kuisaidia Yanga kwani kukosekana kwake tayari kunaonekana kukiathiri kikosi cha Yanga.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema si Chirwa tu anayeidai Yanga lakini wapo wachezaji wengi tu wenye madai lakini hawakugoma.

Amesema wachezaji hao wanamadai sawa na Chirwa (fedha za usajili) lakini wanalipwa mishahara na bonus kila mwezi kwa mujibu wa makubaliano ya mikataba yao.

Mkwasa amebainisha kuwa hakuna mchezaji atakayenyimwa stahiki zake, malipo yamekuwa yakifanywa kwa awamu.Lakini ni muhimu kwa kila mchezaji kuhakikisha anatimiza wajibu wake wakati madai yake yakiendelea kushughulikiwa.

Chirwa alirejea kwao nchini Zambia mwanzoni mwa mwezi Disemba 2017 wakati ligi iliposimama kupisha michuano ya kombe la Chalenji.

Alitarajiwa kurudi wiki iliyopita lakini mchezaji huyo aligoma kurejea hadi atakapolipwa pesa zake zote anazodai.

Mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’