Kuna mabeki wa timu ligi kuu walifurahia kusikia Yanga imemuuza Tuisila Kisinda klabu ya RS Berkane huko Morocco
Kisinda alikuwa akiwapa 'muhaho' walinzi wa timu pinzani kutokana na kasi yake
Lakini hii inaweza kuwa habari mbaya kwao kwani Wananchi wako mbioni kumnasa winga Jesus Moloko kutoka AS Vita

Moloko ni aina ileile ya Kisinda, ana kasi na huyu ni bora zaidi katika eneo la mwisho
AS Vita walimsajili Moloko kuchukua nafasi ya Kisinda alipoondoka msimu uliopita kujiunga Yanga na sasa yawezekana anakuja Tanzania kwa jukumu lilelile
Ndani ya saa 48 hatma ya winga huyu pamoja na nyota wengine wawili itawekwa hadharani
ADVERTISE HERE