Kisinda alipendelea kujiunga na RS Berkane

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2021
Kisinda alipendelea kujiunga na RS Berkane

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amethibitisha kuwa Yanga inamuuza winga Tuisila Kisinda kwenda RS Berkane ya Morocco baada ya makubaliano kufikiwa

Mfikirwa alisema RS Berkane wametoa ofa nzuri ya mshahara kwa Kisinda mwenyewe na upande wao kama klabu pia wameridhishwa na ofa ya takribani Milioni 350 pamoja na ofa ya kwenda kuweka kambi Morocco

Aidha Kisinda aliyekuwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, mwenyewe pia alipendelea kwenda kujiunga na RS Berkane inayonolewa na Florente Ibenge aliyekuwa kocha wake AS Vita

Mashabiki wa Yanga hawakufurahishwa na taarifa hii ya kuuzwa kwa mchezaji wao muhimu ingawa, wakati mwingine ni maamuzi magumu ambayo klabu inalazimika kuyachukua

Kwani kama mchezaji mwenyewe ametaka aruhusiwe akajiunge na RS Berkane, hivyo ni wazi kama Yanga ingegomea ofa hiyo angesubiri mkataba wake umalizike kisha aondoke bure

Uongozi wa Yanga umeahidi watasajili mchezaji mbadala wake, wakiwa na wiki moja tu kukamilisha usajili huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’