Uongozi wa Yanga utakamilisha michakato yote ya usajili wiki hii tayari kwa timu kuingia kambini wiki ijayo, imefahamika
Aidha dirisha la usajili kwa ajili ya michuano ya CAF litafungwa August 15 hivyo Yanga wanakimbizana na muda kuhakikisha wanakamilisha michakato yote kwa wakati
Kesho Jumanne Yanga huenda ikatangaza majina ya wachezaji ambao wameachwa katika kikosi cha msimu ujao
Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji nane Shabani Djuma, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Khalid Aucho na Djgui Diarra
Wengine ni Yusuph Athuman, Dickson Ambundo na Bryson David. Wachezaji 10 huenda wataachwa
ADVERTISE HERE