Yanga imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya hapo jana kumuongeza kikosini mlinda lango Djgui Diarra, nahodha wa timu ya Taifa ya Mali
Mpaka sasa kuna nafasi tatu ambazo bado hazijajazwa kulingana na mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi
Mlinzi wa kati na viungo wawili, mmoja wa ukabaji na mwingine kiungo wa ushambuliaji
Beki wa Kimataifa ya DR Congo Yannick Bangala anatajwa kuwa kwenye rada za Wananchi
Mlinzi huyo aliyekuwa akiitumikia FAR Rabbat kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na klabu hiyo kutoka Morocco
Jana Yannick alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwaaga mashabiki wa FAR Rabbat
Wachezaji kutoka DR Congo wengi wanavutiwa kujiunga na Yanga kutokana na mahusiano mazuri anmbayo Yanga imetengeneza na wachezaji hao
Mukoko Tomombe, Tuisila Kisinda, Shabani Djuma, Fiston Mayele na Heritier Makambo ni mabalozi wazuri wa Yanga huko DR Congo