Kazi inaendelea, wekeni bando

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2021
Kazi inaendelea, wekeni bando

Baada ya mchezo dhidi ya Express Fc hapo jana ambao Yanga iliondoshwa kwenye michuano ya kombe la Kagame kwa kufungwa mabao 3-1, Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz aliwapongeza vijana kwa kuipambania timu licha ya kupoteza mchezo huo

Aidha Nugaz akawaambia Mashabiki kuwa sasa michuano hiyo imemalizika na wanaelekeza nguvu katika ujenzi wa kikosi chao

"Ninachowaambia wanachama na mashabiki wetu sasa waweke bando, tumalizie huku kwenye usajili kwanza," alisema Nugaz

Leo Yanga huenda ikatambulisha usajili wa nyota mwingine wa kigeni ambaye inaelezwa tayari ametua nchini

Nyota wawili wa kigeni waliokuwa wakizungumzwa sana ni mlinda lango kutoka Mali, Diarra Djigui na kiungo mkabaji Khalid Aucho

Djigui ndiye anatajwa kuwa ndani ya viunga vya Avic Town kumalizana na Wananchi wakati Aucho imeelezwa walishamlizana nae na atakuja nchini wiki ijayo

Mlinda lango Djigui anatokea klabu ya Stade Malien ambao ni mabingwa wa Mali

Kipa huyo, mwenye miaka 26, alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanaocheza kwenye ardhi ya nyumbani (CHAN) 2020

Bilionea wa GSM Ghalib Said Mohamed ilibidi apande dau ili kumshawishi kipa huyo aliyekuwa akiwaniwa na timu moja kutoka Afrika Kusini

Djigui alicheza fainali za Kombe la Dunia la Vijana U-20 (2015) na kuiwezesha Mali kumaliza ya tatu nyuma ya Serbia na Brazil, alikuwa mmoja wa makipa watatu bora katika fainali za CHAN 2020 zilizofanyika nchini Cameroon baada ya kuonyesha kiwango kikubwa hasa kuzuia michomo mikali wakifika fainali na kumaliza wa pili nyuma ya Morocco

Kama Wananchi watamtambulisha mlinda lango huyo, itamaanisha Mkenya Farouk Shikhalo hataongezwa mkataba kuendelea kuitumikia Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’