Ali Kiba afunguka Niyonzima kuondoka Yanga, amtakia kila la kheri

Admin By Admin
•
8 Jul 2017
Ali Kiba afunguka Niyonzima kuondoka Yanga, amtakia kila la kheri
Ali Kiba, mkali wa muziki wa kizazi kipya ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Yanga. Mara nyingi Kiba huwa hakosi mechi muhimu za Yanga zinazopigwa kwenye dimba la Taifa.

Kiba na aliyekuwa kiungo wetu fundi Haruna Niyonzima walikuwa marafiki sana. Kama ilivyo kwa Kiba, mara nyingi Niyonzima alikuwa akihudhuria 'show' za mkali huyo wa Bongofleva.

Sasa kuondoka kwa mchezaji huyo Jangwani kimemuumiza sana Kiba kulingana na mahojiano aliyofanya na mtandao wa ShaffihDauda.

“Nimejisikia vibaya kwa sababu mimi ni shabiki wa Yanga namkubali Niyonzima, lakini mpira ni kazi yake unapokuwa unatumikia sehemu kwa muda mrefu inafika kipindi unataka kwenda sehemu nyingine.”

“Kwanza ni historia nzuri kwake kwenye mpira kwamba amecheza klabu fulani na fulani, anatajwa kwenda Simba, ni klabu kubwa vilevile.”

“Nitaendelea kum-support kama mshkaji wangu lakini mimi ni shabiki wa Yanga na sija-mind yeye kutoka Yanga kwa sababu ni moja ya mafanikio kwake ameangalia maslahi na yeye ni mchezaji mpira.”

“Mchezaji mpira anafanana na sisi wanamuziki, tunaangalia panapokuwa na maslahi. Hata leo promota akiniambia ana kiasi hiki halafu mwingine akanipigia simu akaniambia ana zaidi nakwenda kwingine.”

“Vilevile sidhani kama amefanya maamuzi mabaya japokuwa mimi ni mwana Yanga na nilitamani aendelee kubaki Yanga ila ana uhuru.”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
37m ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →