Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zimekubaliana Ligi kusimama kila ambapo timu Tanzania zinazoshiriki michuano ya kimataifa zitakapokuwa na michezo hiyo ya kimataifa ili kuondoa viporo kwa baadhi ya timu hasa zitakazokuwa zinashiriki CAF Champions League na CAF Confederation Cup
Mtendaji wa Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema malengo yao makubwa msimu huu ni kukomesha viporo jambo ambalo limekubaliwa na Wenyeviti wa vilabu vyote vya Ligi Kuu ambao walishiriki kikao na Bodi ya Ligi
Kwa misimu ya karibuni vilabu vilivyokuwa vikishiriki michuano ya CAF hasa Simba, vimekuwa vikirundikiwa viporo hivyo kukosa uwiano mzuri wa ushindani na timu nyingine
Mfano, msimu huu pekee Simba ilikuwa na viporo sita ambapo kuna wakati ligi ilisimama kusubiri wao wacheze michezo yao
Utaratibu huu mpya utapunguza idadi hiyo ya viporo kama sio kuviondoa kabisa