Hali ya mshambuliaji wa Polisi Tanzania Gerrald Mdamu imeelezwa sio nzuri na pengine anahitaji msaada kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu
Mdamu alivunjika miguu yote miwili katika ajali ya basi mwezi uliopita wakati akitoka mazoezini na wachezaji wenzake
Mwanahabari Nestory Tweve alipata nafasi ya kumtembelea Mdamu Hospitalini ambapo ameeleza kuwa hali yake hairidhishi anahitaji msaada hata kwenda kutibiwa nje ya nchi aweze kusimama
Kama umeguswa, unaweza kumfariji Mdamu kwa kumchangia fedha ambazo zitamsaidia katika matibabu yake
Namba ya simu ni 0714716843 (BENEDICTOR MDAMU)
ADVERTISE HERE