Michuano ya kombe la Kagame uongozi wa Yanga unaitumia kimkakati
Moja kuwapa nafasi wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa hawatumiki sana pamoja na timu ya vijana
Baada ya michuano hii kuna wachezaji watabakishwa, wengine watatolewa kwa mkopo na wengine kupewa mkono wa kwaheri
Hivyo michuano hii ni kama nafasi kwa baadhi ya wachezaji kupigania hatma yao kuendelea kuitumikia Yanga
Pili wapo wachezaji wanaangaliwa kupitia michuano hii kabla ya kupewa mikataba
Yanga haikulenga matokeo zaidi ingawa ukiwa mchezaji wa Yanga unapaswa kufahamu ushindi ni kipaumbele cha kwanza
Wachezaji wanaotumika ni wa Yanga na wanapaswa kuipigania timu kupata matokeo
Wale watakaofanya vizuri wanaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha Nasreddine Nabi, lakini wengine wanaweza kutolewa kwa mkopo lakini wale watakaoshindwa kushawishi, wataachwa