Majira ya saa moja usiku pale uwanja wa Benjamin Mkapa, kikosi cha Yanga kitakuwa uwanjani kuikabili Atlabara kutokea Sudan Kusini
Ni mchezo wa pili wa kombe la Kagame kwa Wananchi, leo wakizihitaji alama zote tatu kuweka hai matumaini ya kutinga nusu fainali
Mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya Express dhidi ya Nyasa Big Bullets utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri
Baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo uliopita dhidi ya Nyasa Big Bullets, kiungo mshambuliaji Dickson Ambundo atakuwa uwanjani kuwapa furaha mashabiki wa Yanga
Ambundo alikonga nyoyo za mashabiki wa Yanga katika mchezo wa kwanza ambao alitoa pasi iliyozalisha bao lililofungwa na Waziri Junior

Yeye na kiungo mshambuliaji Jimmy Ukonde walikuwa gumzo baada ya mchezo huo licha ya kuwa ilikuwa mara yao ya kwanza kuvaa uzi wa Yanga
Wachezaji hao walishuka dimbani pasipo kufanya mazoezi na wenzao kwani walitua kikosini siku ambayo mchezo huo ulipigwa
Baada ya kufanya mazoezi na timu kwa takribani siku tatu, Wananchi watarajie ubora zaidi kutoka kwao na kwa kikosi cha Yanga kwa ujumla wake