Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameeleza kuridhishwa na kufanyiwa kazi kwa ripoti ya mapendekezo ya usajili aliyoacha kwa uongozi
Nabi ambaye yuko mapumziko nchini Tusinia, aliacha mapendekezo ya nafasi ambazo alihitaji kuongezewa nguvu
Mpaka sasa Yanga imetambulisha usajili wa wachezaji watatu, Fiston Mayele (Mshambuliaji), Heritier Makambo (Mshambuliaji) na Yusuph Athumani (Mshambuliaji)
Lakini pia wamesajiliwa Dickson Ambundo (winga), Jimmy Ukonde Julio (winga),Β Shabani Djuma (mlinzi) na David Brson (mlinzi)
Pamoja na usajili uliofanyika, Nabi amesema anataka beki mwingine wa kigeni na tayari kuna mmoja ambaye wameshamalizana nae ila bado kuja nchini tu na kutambulishwa
Alisema baada ya hapo kuna maeneo mengine kama katikati pamefanyiwa kazi kwa kuongezwa washambuliaji wawili, Fiston Mayele na Heritier Makambo ambao anaimani wataongeza makali ya nafasi hiyo
"Ukiunganisha nguvu ya wale waliokuwepo msimu uliopita kama Yacouba Sogne mfungaji bora wa timu pamoja na Mayele, Makambo naimani kubwa tutakuwa na safu kali ya ushambuliaji yenye uwezo wa kufunga mabao mengi kuliko msimu huu," Nabi alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
"Tumeimarisha safu yetu ya ulinzi kwa kusajili mabeki wa pembeni ambao naimani nao watakuja kuongeza uimara katika kuzuia na kuifanya timu yetu kutofungika kwa urahisi"
Kocha huyo mwenye uraia pacha wa Ubelgiji na Tunisi, amesema atakuwa na nafasi nzuri na uwanja mpana zaidi kuzungumzia usajili na ripoti yake kiujumla pale dirisha litakapofungwa Agosti 31
Hata hivyo Yanga inapaswa kukamilisha usajili wa michuano ya CAF kabla ya August 15 siku ambayo dirisha la usajili kwa ajili ya michuano hiyo litafungwa