Ni wazi usajili wa Heritier Makambo umekamilisha safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo sasa itakuwa ikiundwa na Yacouba Songne, Makambo, Fiston Mayele na Yusuph Athumani
Yanga inasajili kwa kulingana na mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi ambapo baada ya kuwanasa washambuliaji hao, maboresho mengine yanasubiriwa katika eneo la kiungo na safu ya ulinzi
Dickson Ambundo ni ingizo jipya eneo la winga kama ilivyo kwa Jimmy Ukonde Julio ambaye mabosi wanaendelea kumtazama katika michuano ya kombe la Kagame
Yanga inatarajiwa kusajili viungo wengine wawili, kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji wanaokuja kuchukua nafasi za Carlinhos na Haruna Niyonzima
Aidha katika safu ya ulinzi, beki wa kati raia wa kigeni anatarajiwa kutua kuchukua nafasi ya Lamine Moro huku eneo la ulinzi upande wa kulia ni Djuma Shabani anayesubiriwa huku kushoto mzawa David Bryson anasubiri kutambulishwa
Langoni mlinda lango Mtanzania Erick Johora aliyekuwa akiitumikia Aigle Noir ya Burundi anatajwa kuwa miongoni mwa nyota wapya wanaosubiri kutambulishwa