Baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Yanga, mshambuliaji Yusuph Athumani amesema amejisikia faraja kurejea Yanga
Yusuph amesema Yanga kwake ni nyumbani na hakuna jambo zuri kama kurejea nyumbani
“Nimerudi nyumbani nafurahi tena kuvaa jezi ya Young Africans. Alhamdulillah mimi ni Mwananchi, mimi ni njano na kijani,” alisema Yusuph
Yusuph ni miongoni mwa wachezaji waliolelewa katika timu ya vijana ya Yanga, akicheza pamoja na vijana wengine kama Yusuph Mhilu ambaye yuko Kagera Sugar, Paulo Godfrey, Gustava Simon na wengine wengi
Baada ya kuonyesha kuwango bora na klabu ya Biashara United, umekuwa wakati sahihi kwake kurejea Yanga
ADVERTISE HERE