Jana kiungo Jimmy Julio Ukonde alipata nafasi ya kuitumikia Yanga katika mchezo wa kombe la Kagame dhidi ya Nyasa Big Bullets uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Nyota huyo kutoka klabu ya UD Songo yuko mbioni kujiunga na Yanga lakini usajili wake utakamilishwa baada ya michuano ya Kagame
Ukonde alitua nchini usiku wa kuamkia jana hivyo alishuka dimbani kuikabili Nyasa Big Bullets pasipo kufanya mazoezi na wenzake
Ni wazi mchezo huo wa kwanza hauwezi kuwa kipimo sahihi cha uwezo wake. Alikosa 'match fitnes' pengine kutokana na uchovu
Ni mchezaji anayehitaji kuangaliwa zaidi katika mechi zijazo
Kuna mijadala mingi inaanzishwa na watu wasioitakia mema Yanga, wananchi wanapaswa kuwa makini nayo
Yanga inashiriki michuano ya Kagame kimkakati zaidi kwani michuano hii itawasaidia katika maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao