Moja ya sajili bora ambayo viongozi wa Yanga wanastahili pongezi kuikamilisha ni hii ya mshambuliaji Fiston Mayele kutoka klabu ya AS Vita
Kwa misimu miwili iliyopita, Yanga imekuwa na changamoto kwenye safu yake ya ushambuliaji
Tangu alipoondoka Makambo, Yanga haikuweza kupata mshambuliaji wenye uwiano mzuri wa kuzifumania nyavu
Ujio wa Fiston unakwenda kumaliza changamoto hiyo, kwani huyu ni straika wa mabao
Takwimu zake katika msimu uliopita znadhihirisha yeye ni mchezaji wa aina gani
Katika msimu uliopita kwenye ligi DR Cong, Fiston alifunga mabao 13 katika michezo 26 huku akipachika mabao matatu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambapo kwenye hatua ya makundi alifunga bao moja na kutengeneza nafasi moja wakati raundi ya kwanza alifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao
Huyu ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya DR Congo pia, wengi watakumbuna kabla ya michuano ya CHAN iliyofanyika Cameroon, DR Congo walikuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kirafiki
Fiston alifunga bao la Congo katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Aidha kucheza na Shabani Djuma, Mukoko Tomombe na Tuisila Kisinda ambao alikuwa nao AS Vita ni faida nyingine kwake
Mukoko na Kisinda watamsaidia kuzoea haraka ligi ya Tanzania kwani hata ujio wake umechangiwa na ushawishi wa wachezaji hawa