Kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama anaendelea na program za mazoezi aliyoachiwa na Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi
Balama amepona majeraha yaliyomuweka nje mwaka mzima, ni suala la muda tu ataanza kuonekana uwanjani
Aidha imeelezwa kuwa nyota huyo anaweza kuwa na dakika zake kwenye michuano ya Kagame inayoanza leo jijini Dar es salaam
Ni faraja kumuona Balama akirejea tena uwanjani baada ya kupona majeraha yaliyoweka hatarini maisha yake ya kusakata kabumbu
ADVERTISE HERE