Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania umri chini ya miaka 23 kimefanikiwa kushinda taji la CECAFA Challenge U23 baada ya kuichapa Burundi kwa mikwaju ya penati 6-5
Ni katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo iliyopigwa nchini Ethiopia ambao dakika 90 zilimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Ni taji la kwanza kwa kocha Kim Poulsen aliyerejea mapema mwaka huu kuinoa Tanzania
Mlinda lango Metacha Mnata alikuwa bora langoni leo akichangia Tanzania kuweza kushinda taji hilo
Pongezi nyingi kwao kwa kufanikiwa kushinda taji hilo
ADVERTISE HERE