Yanga imekamilisha usajili wake kwa asilimia 90 hata hivyo bado uongozi haujaweka wazi nyota ambao watawatumikia mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao
Kuna wachezaji wengi wamehusishwa na Yanga, baadhi yao yawezekana wakasajiliwa lakini wengini zinabaki kuwa tetesi mpaka pale uongozi utakapotangaza rasmi
Hapa tunagusia nyota wa kigeni ambao baadhi yao wanahusishwa kuwa wataitumikia Yanga msimu ujao
1. Djuma Shabani
Huu ni usajili ambao pamoja na kuwa bado haujatangazwa, tayari umekamilika
Taarifa za usajli wa Djuma mlinzi wa kulia aliyekuwa akiitumikia AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo, zilithibitishwa na yeye mwenyewe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Djuma ni miongoni mwa wachezaji waliong'ara kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita
2. Fiston Mayele
Ni mshambuliaji kutoka klabu ya AS Vita. Msimu uliopita Mayele alifunga mabao 13 katika ligi kuu ya DR Congo akiwa pia mchezaji wa timu ya Taifa ya DR Congo
Naye hakuficha ujio wake Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akiwataja Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda kuwa wachezaji waliomshawishi kutua Jangwani
3. Heritier Makmbo
Hili sio jina geni kwa mashabiki wa Yanga. Wiki iliyopita alitangaza kuvunja mkataba wake na Horoya Ac na matarajio ya wengi ni kuwa atarejea katika klabu aliyopata mafanikio misimu miwili iliyopita
Makambo tayari ana uzoefu wa ligi ya Tanzania, wengi wanaamini ni mchezaji sahihi kujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao
4. Francis Kazadi Kasengu
Ni winga/mshambuliaji Mcongomani ambaye jina lake limetajwa katika usajili wa Yanga msimu huu
Anacheza klabu ya Al Masry ya nchini Misri akitokea klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco. Naye amewahi kuitumikia klabu ya AS Vita
5. Tape Eliezer
Huyu hafahamiki sana na Wananchi lakini ni mlinda lango mahiri wa klabu ya San Pedro Fc. Ni raia wa Ivory Coast ambaye tetesi zinabainisha kuwa huenda akatua kuchukua nafasi ya Farouk Shikhalo aliyemaliza mkataba
6. Partene Counou
Huyu ni mlinzi wa kati kutoka nchini Benin ambaye anatajwa kuja kuchukua mikoba iliyoachwa na Lamine Moro aliyeachwa
7. Halid Aucho
Ni mchezaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Uganda ambaye hucheza nafasi ya kiungo. Aucho anatajwa kuwa mrithi wa Calinhos aliyeondoka Yanga mwezi April
8. Justice Blay
Ni kiungo mkabaji kutoka nchini Ghana, msimu uliomalizika aliibuka kuwa kiungo bora wa ligi ya Ghana. Yanga imedhamiria kuimarisha eneo la kiungo cha ukabaji kwa kuwaongezea nguvu Mukoko Tonombe na Zawadi Mauya
9. Kwame Bonsu
Kiungo mwingine raia wa Ghana, fundi haswa anayeweza kufananishwa na Haruna Niyonzima enzi za ujana wake. Huyu anatajwa kuwa mrithi halisi wa Niyonzima
Inaelezwa Yanga itasajili wachezaji saba wa kigeni huku ikitarajiwa kusalia na wachezaji wa tatu waliyoitumikia msimu uliopita kufanya idadi ya wachezaji wa kigeni kuwa 10