Kibwana ndiye mchezaji bora chipukizi msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jul 2021
Kibwana ndiye mchezaji bora chipukizi msimu huu

Ukizungumzia wachezaji waliong'ara katika kikosi cha Yanga kwenye msimu huu uliomalizika, hutakosa kutaja jina la Kibwana Shomari

Mlinzi kinda aliyesajiliwa na Wananchi akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, amewafanya mashabiki wa Yanga wamsahau mkongwe Juma Abdul haraka sana

Ndio! Abdul alikuwa roho ya Yanga upande wa kulia kwa takribani misimu minne kabla ya kugomea mkataba aliopewa kuelekea msimu wa 2020/21

Na hapo ndipo akaletwa Kibwana katika nafasi yake, msimu wake mmoja umetosha kudhihirisha kipaji chake

Ni kinda mwenye umri wa miaka 20 tu, lakini amekuwa nguzo muhimu ya safu ya ulinzi upande ule wa kulia

Kibwana ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga msimu huu

Ameng'ara katika mechi zenye ushindani zaidi dhidi ya Simba akiweza kuwadhibiti nyota wanaotegemewa na timu hiyo

Kwa hakika ni mchezaji anayestahili tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika tuzo za VPL msimu huu

Msimu ujao anatarajiwa kupata ushindi katika nafasi yake mbele ya Shabani Djuma anayetua kutoka klabu ya AS Vita

Djuma ni mchezaji mzoefu, hakuna shaka ujio wake utamuimarisha zaidi Kibwana

Lakini jambo jema zaidi ni kuwa Djuma pia anaweza kucheza nafasi ya winga, hivyo Kibwana bado atakuwa na uhakika wa muda wa kutosha kikosini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’