Ni kweli Chirwa anaidai Yanga - Sanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jan 2018
Ni kweli Chirwa anaidai Yanga - Sanga
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amekiri mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa amegoma kushinikiza alipwe fedha zake za usajili.

Akizungumza kwenye mkutano wa wanachama wa matawi mkoa wa Mwanza uliofanyika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Nyamagana Ijumaa iliyopita, Sanga amesema ni kweli Chirwa amegoma kwa sababu anadai kiasi cha fedha ambacho hakukiweka wazi.

Yanga iko visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

"Hawa wachezaji tunaishi nao kama watoto wetu, tunafahamu na wenyewe ni binadamu kama sisi na wana maisha nje ya soka. Ni kweli tunadaiwa na Chirwa ila anatudai fedha za usajili pekee ambayo tulitakiwa kumlipa baada ya sisi kumsajli," alisema Sanga

Aidha, Sanga amekanusha madai kwamba kuna wachezaji wanadai mishahara, kwani wametumia zaidi ya Sh. Milioni 100 kulipa mishahara yote ya wachezaji hadi mwezi Novemba 2017 na sasa wanatayarisha mishahara ya Desemba.

Sanga amewaomba wanachama wa Yanga watulia na kuacha kusikiliza maneno ya kwenye mitandao, badala yake wafanye kazi ya kuijenga klabu yao na waache malumbano.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’