Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumapili, Julai 25 katika uwanja wa Lake Tanganyika
Akizungumzia kuhusu maandalizi ya kikosi chake, Nabi amesema wamejiandaa kwa mazingira yoyote watakayokutana nayo katika mchezo huo
"Hali ya hewa hapa Kigoma sio nzuri sana lakini pia sio mbaya, kikubwa tumejiandaa kwa hali yoyote kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba. Nawashukuru mashabiki wetu hapa wametupokea vizuri, " alisema Nabi
Aidha kocha huyo raia wa Tunisia amethibitisha kuwa watamkosa kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye alipata majeraha wakati wa maandalizi kuelekea mchezo huo
"Ni kawaida, inapofika mwishoni mwa msimu kunakuwa na uchovu na majeruhi wengi, Saido lipata majeraha mazoezini hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo lakini wachezaji wengine wote wako sawa tayari kwa mchezo"