Safari ya Yanga fainali ASFC ilikuwa kibabe zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2021
Safari ya Yanga fainali ASFC ilikuwa kibabe zaidi

Safari ya Yanga kutinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ilikuwa ya kipekee kwani mabingwa hao wa kihistoria hawakuruhu bao lolote katika michuano hiyo

Aidha ukiondoa mchezo dhidi ya Ken Gold ambao ulifanyika jijini Dar es salaam, mechi zote zilizofuata Yanga walicheza mikoani

Yanga walipaswa kuanza kampeni yao kwa kuikabili Singida United hata hivyo walivushwa raundi hiyo pasipo kucheza baada ya Singida United kushushwa madaraja mawili

Mchezo uliofuata ulikuwa dhidi ya Ken Gold uliopigwa uwanja wa Uhuru na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Lilikuwa bao la mkwaju wa nje ya 18 kutoka kwa mkongwe Haruna Niyonzima 'Fabregas'

Mchezo uliofuata walikwenda Rukwa, Sumbawanga na wakafanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons

Wakaelekea Shinyanga kuikabili Mwadui Fc katika mchezo ambao waliibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 na kutinga nusu fainali

Mechi ya nusu fainali ikapigwa mkoani Tabora wakiichapa Biashara United bao 1-0 na kutinga fainali

Yanga imefunga mabao matano pasipo kuruhusu bao kutikisa nyavu zake

Keshokutwa Jumapili wanakutana na watani zao Simba katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma

Ukiacha mchezo wa nusu fainali ambao ulipangwa kupigwa Songea, mechi nyingine zote Simba walicheza jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’