Aliyekuwa mshambuliaji wa Horoya Ac Heritier Makambo amethibitisha kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande mbili
Makambo alisajiliwa na Horoya Ac mwaka 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea klabu ya Yanga
Nyota huyo amesema alilazimika kuvunja mkataba wake baada ya ujio wa kocha mpya ambaye hakumpa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza
"Maisha yalikuwa mazuri tu pale Horoya ila mara baada ya kocha kubadilishwa na kuja kocha mpya ndio shida ilipoanzia,akaanza niweka benchi so kutokana na quality yangu kwakweli nilikuwa naumia sana juu ya kukaa benchi"
"Basi nikaamua tu kukaa na kuvunja mkataba kwa maelewano ya pande zote mbili. Sababu yangu yakutoka sio sababu nimepata timu Nyingine ila nime vunja mkataba tu kwa maisha maana heshima ni zaidi ya pesa," Makambo alisema katika mahojiano na SportExtra
Aidha akizungumzia tetesi za kutakiwa na Yanga, Makambo amesema kwa sasa yeye ni mchezaji huru na hatakuwa na kinyongo kujiunga na waajiri wake hao wa zamani kwani alifurahia maisha yake ya soka wakati akiwa Yanga
"Ninazo ofa nyingi lakini siwezi taja timu ambazo zimenifuata,Tanzani a ni nchi yangu ya pili maana pale nimeishi kwa raha sana"
"Yanga ni timu yangu naipenda na ikitokea wamehitaji huduma yangu basi nitakwenda na nitapambana kwa kila namna nifanye vizuri zaidi ya kipindi kile," alisema Makambo