Habari za uhakika ni kuwa mlinzi aliyesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya AS Vita Shabani Djuma anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Alhamisi
Djuma huenda akajumuishwa kwenye msafara wa Yanga utakaoelekea mkoani Kigoma kushuhudia mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili, Julai 25
Aidha nahodha huyo wa zamani wa AS Vita, anaweza kuwasili nchini akiongozana na mshambuliaji Fiston Mayele
Mkataba wa Mayele na AS Vita unamalizika leo, huenda baada ya hapo Yanga itakuwa huru kuweka wazi usajili wa mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 13 kwenye ligi kuu ya DR Congo msimu uliomalizika
Wananchi wanasubiri kwa hamu utambulisho wa nyota hao pamoja na wengine wapya watakaokuwa wamesajiliwa
ADVERTISE HERE