Kesi ya Morrison kuanza kuunguruma leo CAS

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jul 2021
Kesi ya Morrison kuanza kuunguruma leo CAS

Kesi ya Bernard Morrison na Yanga inaanza kusikilizwa kuanzia leo katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS)

Kesi hiyo yenye namba CA S2020/A/739, itasikilizwa na Jaji Patrick Stewart kutoka Uingereza na inatarajiwa kusikilizwa kwa njia ya mtandao

Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa tayari walishawasilisha nyaraka muhimu zilizotakiwa na Mahakama hiyo

"Mahakama ilituamuru tuandae ushahidi wa kiapo cha Injinia Hersi Said na kuutuma CAS. Tayari klabu imefanya hivyo na kesho (leo) kesi hiyo itasikilizwa mbele ya Jaji Patrick Stewart raia wa Uingereza," Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa alinukuliwa na gazeti la Mwananchi

Katika kesi ya msingi, Yanga inapinga uamuzi uliotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kubatilisha mkataba wa miaka miwili ambao Morrison alisaini na Yanga baada ya mkataba wa awali wa miezi sita kumalizika

Morrison alikana kusaini mkataba huo lakini Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji katika hukumu yake ilikiri kuwepo kwa mkataba lakini ikadai ulikuwa na mapungufu

Mwanasheria wa Yanga Alex Mgongolwa anayesimamia kesi hiyo, alieleza kuwa kesi ya msingi ilikuwa kubaini kama Morrison alikuwa na mkataba na Yanga au la, Kamati ilijiridhisha kuwa alisaini mkataba hivyo ilipaswa kuishia hapo, suala la mapungufu ya mkataba halikuwa kesi ya msingi na lilihusu pande zilizoingia mkataba huo

Mgongolwa pia alibainisha kuwa hata mapungufu yaliyotajwa sio miongoni mwa sababu zinazoweza kubatilisha mkataba kwa mujibu wa sheria

Zaidi Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilimuagiza Morrison kurudisha fedha dola 30,000 alizokuwa amechukuwa Yanga na wakati huo ikimtangaza kuwa mchezaji huru

Aidha Morrison alionekana akisaini mkataba na klabu ya Simba hata kabla hukumu ya kesi hiyo haijatolewa na pamoja na mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya Maadili kutaka mchezaji huyo achukuliwe hatua, hakuna kilichofanyika

Miezi michache nyuma kabla ya sakata hilo, Morrison alitoa malalamiko juu ya aliyemtaja kuwa Wakala wa Simba kumpa hongo ya Dola 5,000 ili akasaini mkataba na klabu ya Simba

Yanga ilipeleka Malalamiko TFF juu ya tuhuma hizo lakini hakuna kilichofanyika na baadae Kamati ya TFF ikabatilisha Mkataba wake na Yanga siku chache tu tangu Morrison aonekane anasaini mkataba na Simba

Ndipo Yanga ikafungua kesi (CAS) wakiamini baada ya kukosa haki yao kwenye mamlaka za ndani za usimamizi wa soka wanaweza kuipata huko katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo

Kesi inatarajiwa kusikilizwa kwa siku mbili, pengine hukumu inaweza kutolewa wiki hii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’