Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2020/21 inamalizika leo ambapo kwa Yanga msimu watamaliza wiki ijayo baada ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa iuwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma
Ni wazi kuchelewa kumalizika kwa ligi, kunaweza kuathiri maandalizi kuelekea msimu ujao
Uongozi wa Yanga umepanga kuwapa wachezaji mapumziko ya wiki mbili tu baada ya fainali ya FA
Yanga itaanza maandalizi ya msimu wa 2021/22 mwanzoni mwa mwezi wa nane
Mabingwa hao wa kihistoria, watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao ambapo kalenda ya michuano hiyo inaonyesha kuwa mechi za hatua ya awali zitapigwa mwanzoni mwa mwezi Septemba 2021
Wananchi watakuwa na takribani mwezi mmoja tu wa kujiandaa na michuano hiyo na bila kusahau kutakuwa na tukio la wiki ya Mwananchi katikati