Kikosi cha Yanga tayari kiko mkoani Dodoma ambapo kesho Jumapili Julai 18, wanakamilisha msimu kwa kuwakabili Dodoma Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri
Mkufunzi wa makipa, Razak Siwa amesema pamoja na kuwa mchezo huo ni wa kukamilisha Ratiba tu, wamedhamiria kuwapa furaha mashabiki wa Yanga mkoani Dodoma kwa kuibuka na ushindi
"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hii ya mwisho na Dodoma Jiji. Ligi ni mbio hivyo sisi tumekuja kupambana kuhakikisha tunamaliza msimu na alama tatu"
"Tunawashukuru mashabiki wetu kwa kuendelea kutusapoti, waje kwa wingi uwanjani. Tunafahamu Dodoma Jiji ni timu nzuri, tumejiandaa kuwapa furaha kwa kuondoka na alama zote tatu," alisema Siwa
Ushindi walioupata Yanga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ihefu Fc, uliwahakikishia Wananchi kumaliza katika nafasi ya pili na hivyo kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Hivyo mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ni wa kukamilisha ratiba tu kwa Wananchi