Metacha ajumishwa kikosi cha timu ya Taifa U23

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2021
Metacha ajumishwa kikosi cha timu ya Taifa U23

Mlinda lango Metacha Mnata ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa U23 ambayo itashiriki michuano ya CECAFA Challenge U23

Metacha amemaliza adhabu ya michezo mitatu aliyokuwa amefungiwa na Bodi ya ligi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Yanga walishinda mabao 3-2

Nyota huyo pia alisimamishwa na uongozi wa Yanga huku hatma yake ikiwa bado mikononi mwa mabosi wake

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Kim Poulsen, ameita wachezaji 20 watakaoingia kambini Julai 19 kujiandaa na michuano hiyo itakayofanyika Ethiopia kuanzia Julai 28

1. Metacha Mnata – Yanga.
2. Daniel Mgore – Biashara United.
3. Wilbol Maseke – Azam.
4. Israel Mwenda – KMC.
5. Nickson Kibabage – Youssoufia (Morocco)
6. Lusajo Mwaikenda – KMC.
7. Sospeter Israel – Azam.
8. Oscar Masai – Ihefu.
9. Lucas Kikoti – Namungo.
10. Joseph Mkele – Mtibwa Sugar.
11. Rajabu Athuman – Gwambina.
12. Meshack Abraham – Gwambina.
13. Reliants Lusajo – Namungo.
14. Erick Mwijage – Kagera Sugar.
15. Andrew Simchimba – Ihefu
16. Abdul Suleiman – Coastal Union.
17. Pascal Msindo – Azam.
18. Abdulrazack Hamza – Mbeya City.
19. Abdulmajid Mangalo – Biashara United.
20. Yusuph Mhilu – Kagera Sugar.

Aidha, Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, timu zinaruhusiwa kuwa na wachezaji watatu wenye umri zaidi ya miaka 23, na hivyo Pulsen amewajumuisha Sospeter Israel, Reliants Lusajo na Yusuf Mhilu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’