Mmoja anahitajika hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2021
Mmoja anahitajika hapa

Maboresho ya safu ya ushambuliaji kwenye kikosi cha Yanga sio jambo lenye mjadala kwani ni eneo lililowakosesha furaha Wananchi msimu huu

Yacouba Songne ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mabao 10 katika mashindano yote

Pamoja na kuwa sio takwimu za kujivunia sana, lakini angalau Wananchi wameielewa kazi yake uwanjani

Michael Sarpong ameshindwa kuonyesha makali yake akimaliza msimu na mabao manne

Ni hivyo hivyo kwa Fiston Abdulrazak aliyetua kwenye usajili wa dirisha dogo, ameondoka akiwa amefunga mabao mawili

Ni wazi Yanga inahitaji kusajili washambuliaji mahiri zaidi ambao wataleta matokeo chanya uwanjani

Mpaka sasa ni tetesi tu zinazovuma, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM injinia Hersi Said akiwahakikishia Wananchi kuwa wanaleta watu hasa wa kazi ambao watazichakaza nyavu za wapinzani

Washambuliaji hawa watatu wanatajwa zaidi, pengine mmoja kati yao au wawili wanaweza kuongoza safu ya Yanga msimu ujao

Heritier Makambo

Heritier Makambo sio mgeni kwa Wanayanga. Bado anaendelea kukumbukwa kwa kazi nzuri aliyofanya msimu wa 2018-19

Yanga ilimuuza Horoya Ac miaka miwili iliyopita, akiwa ametumika kwa msimu mmoja tu

Katika msimu huo, Makambo aliweza kufunga mabao 22 katika mashindano yote

Hakuwa na wakati mzuri sana katika klabu ya Horoya, lakini Wananchi wanaamini akirejea, makali ya safu ya ushambuliaji yatarudi kwani tayari anaifahamu ligi ya Tanzania

Katika moja ya mahojiano, Injinia Hersi alisema wanatambua Wananchi wanamtaka kwelikweli Makambo lakini bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Horoya hivyo wasubiri kuona kama itawezekana kumpata

Fiston Mayele

Mayele ni mshambuliaji wa AS Vita, kule ambako juzi tu Yanga imekamilisha usajili wa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Shabani Djuma

Mayele alishika nafasi ya pili katika mbio za ufungaji bora ligi kuu ya DR Congo msimu uliomalizika akiweka kambani mabao 13

Anacheza timu ya Taifa ya DR Congo na hata walipokuja Tanzania kucheza mechi ya kirafiki hivi karibuni, ni yeye aliyefunga bao la DR Congo katika mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Jean Makusu Mundele

Ni mchezaji mwingine wa AS Vita ambaye msimu uliomalizika aliitumikia Orlando Pirates kwa mkopo

Msimu wa 2018-19, Makusu aliifungia AS Vita mabao 44 katika mashindano yote na haikushangaza kwake kupata nafasi kusajiliwa na Pirates

Pia amewahi kucheza Ligi Kuu ya Ubelgiji klabu ya Standard Liege. Makusu yuko nchini na Inaelezwa aliletwa na Simba lakini mwenyewe ametamani zaidi kujiunga na Yanga ambako tayari wapo wachezaji Wacongoman wenzake aliokuwa nao AS Vita ambao ni Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na Shabni Djuma akiwa njiani kujiunga nao

Aidha majeraha aliyopata msimu uliopita yalimuathiri kwa kiasi na pengine ndio maana hakun'gara Orlando Pirates ambayo awali ilimchukua kwa mkopo ikiwa na lengo la kumsajili moja kwa moja

Hata hivyo usajili wa yeyote utategemea na mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi ambaye ndiye mwenye kauli ya mwisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’