Yanga imetakata uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo wakiichapa Ihefu Fc mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu hatua ya lala salama
Mchezo huo ulitumika kumuaga kiungo Haruna Niyonzima ambaye ameishi vyema na Wananchi
Mabao mawili yaliyofungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' yametosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu ambao umewapa uhakika wa kumaliza kwenye nafasi ya pili

Kwa maana rasmi sasa Yanga itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Kinachofuata uwanja wa Benjamin Mkapa ni hafla ya kumuaga Niyonzima
Kila la kheri Niyonzima, Wananchi tutaendelea kukumbuka mchango wako..
ADVERTISE HERE