Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga, yuko nchini Morocco kwa mwaliko maalum wa klabu ya Raja Casablanca
Mapema mwaka huu, Yanga na Raja Casablanca ziliingia makubaliano ya ushirikiano ambapo safari hiyo ya Hersi ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano hayo
Akiwa Morocco, Injinia Hersi anatarajiwa kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea vituo vya michezo vinavyomilikiwa na Raja
Zipo tetesi kuwa mwamba anaweza kurejea na 'kifaa' kutoka nchini Morocco ingawa mwenyewe amesisitiza safari yake ni ya kikazi zaidi
Aidha Injinia Hersi amedokeza kuwa upo uwezekano Yanga itaelekea nchini Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya kuelekea msimu ujao
Jambo hilo huenda likawa sehemu ya ajenda atakapokutana na mabosi wa Raja