Yanga kutinga Kigoma mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2021
Yanga kutinga Kigoma mapema

Kikosi cha Yanga kitakamilisha ratiba ya ligi kuu Julai 18 mkoani Dodoma kwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri

Leo Wananchi wanakamilisha mchezo wao wa mwisho nyumbani msimu huu kwa kuikabili Ihefu Fc mchezo ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baada ya mchezo wa mkoani Dodoma watakamilisha maandalizi yao ya mwisho jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Kigoma tayari kwa mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba. Mchezo huo utapigwa Julai 25 katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Bumbuli amesema wanatarajia kuwasili mkoani Kigoma Julai 22, siku tatu kabla ya mchezo ili kuwapa wachezaji muda wa kuzoea mazingira

Bosi huyo wa Kitengo cha Habari klabu ya Yanga, amesema wamedhamiria kushinda taji la FA, wana imani kubwa kuwa watafanikiwa

"Tumepanga kufika mapema siku tatu kabla ya mchezo ili kuwapa fursa wachezaji kuzoea hali ya hewa pamoja na benchi la ufundi kutoa mbinu za mwisho kabla ya mchezo wenyewe ambao tumejipanga kuhakikisha tunashinda," alisema Bumbuli.

Aidha Bumbuli amesema watakwenda Kigoma na kikosi cha wachezaji wote ambao wamesajiliwa na lengo kubwa siyo kushinda tu taji hilo, lakini pia kuwapa burudani mashabiki wao wa Kigoma ambao hawajaiona timu yao kwa muda mrefu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’