Kesho Wanayanga watamuaga kiungo Haruna Niyonzima baada ya utumishi wa misimu sita wenye mafanikio makubwa
Niyonzima alitua mwaka 2012 akiwa kijana mdogo, leo baada ya miaka tisa anaondoka huku akiacha heshima kubwa Jangwani
Katika utumishi wake wa awamu mbili ndani ya Yanga, Niyonzima amekusanya jumla ya mataji 11
Fundi huyo wa mpira ameshinda Mataji matano ya Ligi Kuu, Mataji matatu ya Ngao ya Jamii, Mataji mawili ya michuano ya CECAFA pia akishinda taji moja la FA na kombe la Mapinduzi

Mwaka 2017 aliondoka Yanga na kujiunga na Simba, huko nako akishinda mataji mawili ya ligi kuu
Ni uhamisho uliowaumiza sana mashabiki wa Yanga, lakini aliporejea mwishoni mwa mwaka 2019, alieleza waziwazi alilazimika kujiunga na Simba kutokana na maslahi lakini moyo wake ulikuwa Yanga
Niyonzima anaondoka Yanga huku akipewa heshima stahili, mchango wake kwa klabu hii yenye historia ya kipekee, utaendelea kukumbukwa