Kocha wa makipa klabu ya Yanga Razak Siwa amesema wamekamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Akizungumza katika kikao cha mechi mapema leo, Siwa amesema bado hawajakamilisha msimu hivyo wanahitaji kushinda mechi zote zilizobaki
"Tumejiandaa vizuri kwa mechi ya kesho, hatuwezi kuidharau Ihefu sababu ipo chini tuliona mechi dhidi ya Mwadui walitusumbua sana na tayari walikuwa wameshuka daraja"
"Kwetu Ligi bado haijaisha mpaka mwisho kwa hiyo tunahitaji alama tatu kwenye kila mchezo," alisema Siwa
Awali mchezo huo ulipaswa kupigwa leo lakini Bodi ya ligi ilisogeza mbele kwa siku moja michezo yote iliyopaswa kupigwa leo kufuatia klabu ya Polisi Tanzania kupata ajali mkoani Kilimanjaro
Muda wa mchezo huo pia umebadilika kutoka saa moja usiku na sasa utapigwa saa kumi jioni