Akihojiwa na kituo kimoja cha redio mapema leo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said amesema michakato ya usajili itawekwa haradhani baada ya msimu wa ligi kuu kumalizika
Ligi itafikia tamati Jumapili Julai 18 ambapo Yanga itamaliza ratiba yake mkoani Dodoma kwa kuikabili Dodoma Jiji
Baadae Wananchi wataelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa fainali ya FA dhidi ya Simba utakaopigwa Julai 25
Injinia Hersi amesema wanayo orodha ya wachezaji ambao wanamaliza mikataba, hatma yao itafahamika baada ya ligi kumalizika
"Ni kweli kuna wachezaji ambao wanamaliza mikataba, tunasubiri mpaka ligi iishe ndipo tunaanza kufanyia kazi mapendekezo ya Mwalimu juu ya wachezaji ambao anahitaji kuendelea nao, alisema Hersi"
Kuhusu mwenendo wa usajili, Hersi amesema wanaendelea kushirikiana na maskauti wakubwa barani Afrika ili kupata wachezaji wenye ubora
Lakini pia akadokeza kuwa wana jambo lao kule Burundi ambapo wako mbioni kusajili mchezaji mmoja
"Tunafanya kazi vizuri sana na maskauti bora kabisa barani Afrika na muda sio mrefu kuna jambo letu tutaliweka sawa kwa kuwa tunakamilisha mambo madogo na klabu moja ya nchini Burundi"
Tetesi zinadai nyota huyo ni mlinda lango Mtanzania Erick Johola anayeitumikia klabu ya Aigle Noir
Johola alikuja na timu hiyo kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi mwezi August mwaka jana Yanga ikishinda mabao 2-0