Kiungo Deus Kaseke amesema wataendelea kumkumbuka na kumuenzi Haruna Niyonzima kwa mema aliyoifanyia klabu ya Yanga na mchezaji mmoja mmoja
Niyonzima anamaliza mkataba na Yanga ambapo kesho Alhamisi ataagwa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc
Kaseke amecheza na Niyonzima katika awamu mbili tofauti
Awamu ya kwanza ni wakati Yanga ikiwa chini ya kocha Hans van De Pluijm msimu wa 2015/16 na 2016/17
Awamu ya pili ni msimu wa 2019/20 na msimu huu unaomalizika Jumapili
Kaseke amemtaja Niyonzima kama mchezaji kiongozi aliyekuwa akiwaunganisha wachezaji wote
Amesema nyota huyo wa Kimataifa kutoka Rwanda, amekuwa msaada kwa wachezaji wenzake nje ya soka
ADVERTISE HERE